Kocha wa Kenya U20 asherehekea ‘bathidei’ kibarua cha Namibia kikinukia – Taifa Leo


Kocha wa Kenya U20 asherehekea ‘bathidei’ kibarua cha Namibia kikinukia

Kocha wa Kenya U20 asherehekea ‘bathidei’ kibarua cha Namibia kikinukia

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, Curtis Olago Aluoch amesherehekea kufikisha umri wa miaka 41 mnamo Aprili 24, 2023.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Impala Saracens, Nondescripts na Kenya Business Financial institution amesherehekewa kwa wimbo na vijana wake waliozaba Uganda 44-20 na kufuzu Aprili 22 kushiriki nusu-fainali ya Kombe la Afrika (U20Barthes Trophy) dhidi ya Nambia itakayosakatwa Aprili 26.

Olago anayefahamika kwa majina ya utani kama Colago ama 001, alizaliwa Aprili 24, 1981 katika kaunti ya Siaya.

Alisomea shule ya upili ya Nairobi College inayofahamika sana kwa mchezo wa raga ambako alianzia uchezaji wake akiwa katika kidato cha kwanza mwaka 1997.

Alianza kutia klabu ya KCB makali mwaka 2012. Alishinda Ligi Kuu (Kenya Cup) kwa mara ya kwanza kama kocha msimu 2014-2015 wakati KCB ililemea Kabras Sugar 27-3.

Olago ameongoza KCB pia kutawala ligi msimu 2016-2017, 2017-2018, 2018-2019 na 2021 pamoja na Kombe la Enterprise 2015, 2016, miongoni mwa mataji mengine.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Articles