Azimio kurejelea maandamano jijini Nairobi – Taifa Leo


Azimio kurejelea maandamano jijini Nairobi

Azimio kurejelea maandamano jijini Nairobi

NA CHARLES WASONGA

MUUNGANO wa Azimio La Umoja-One Kenya umetangaza utarejelea maandamano ya amani Jumanne wiki ijayo, Mei 2, 2023.

Kwenye taarifa Jumatatu Aprili 24, 2023, Mwenyekiti wa Baraza kuu la muungano huo, Wycliffe Ambetsa Oparanya anasema wameamua kurejelea maandamano baada ya kubaini kuwa Kenya Kwanza ‘haina nia njema’ katika kufanikisha mazungumzo.

“Kwa mfano Kenya Kwanza inasisitiza kuwa sharti mbunge wa Eldas Aden Keynan ashirikishwe katika timu yake ya washiriki wa mazungumzo ilhali kisheria yeye ni mwanachama wa Azimio,” Bw Oparanya anasema katika taarifa hiyo.

Gavana huyo wa zamani wa Kakamega anasema kwa kujumuisha Keynan katika kundi lake, Kenya Kwanza imeonyesha wazi kuwa haiheshimu misingi ya Demokrasia ya vyama vingi, mojawapo ya masuala ambayo Azimio inalalamikia.

Bw Oparanya pia ameongeza kuwa Kenya Kwanza haijaonyesha nia na kujitolea kwake kupunguza bei ya unga, umeme, mafuta na karo.

“Wameamua kuingiza propaganda katika suala hili muhimu ilhali Wakenya wanaendelea kuumia,” Bw Oparanya akasema.

Na tofauti na maandamano ya mwezi Machi, Bw Oparanya anasema maandamano yanayoanza Mei 2, 2023 yatajikita jijini Nairobi pekee.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Articles