Timu zaendelea kupigana mbio za taji zikiwa za Gaspo Girls na Vihiga Queens – Taifa Leo

[ad_1]

KWPL: Timu zaendelea kupigana mbio za taji zikiwa za Gaspo Women na Vihiga Queens

KWPL: Timu zaendelea kupigana mbio za taji zikiwa za Gaspo Girls na Vihiga Queens

AREGE RUTH NA OSBORN MANYENGO

GASPO Girls iliendelea kuganda kileleni mwa Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Trans Nzoia Falcons katika uwanja wa Ndura mjini Kitale mnamo Jumapili.

Warembo wa Falcons walikosa kumalinika nyumbani safu ya kati na ya nyuma, jambo lililowapa wageni nafasi ya kutawala kipindi cha kwanza.

Timu zilienda mapumziko Gaspo ikiwa kifua mbele kwa magoli mawili yaliyofungwa na Diana Wachera na Wambui Elizabeth.

Kipindi cha pili Falcons yake Justin Okiring, walijaribu kujikaza na kupata goli kupitia kwa mshambulizi Joyce Makungu. Bao la tatu la Gaspo lilitiwa wavuni na Diana Wachera na kuzamisha meli ya Falcon nyumbani.

Gaspo ambao wanapanga kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, wanaongoza kwenye msimamo wa ligi na alama 37 sawa na Vihiga Queens lakini wanatofautiana na mabao manne.

Tangia kujiunga na KWPL mwaka 2018, Gaspo hawajawahi kutwaa ubingwa wa ligi.

Kabla ya mechi hiyo, Aprili 17, 2023 Gaspo pamoja na Vihiga walibanduliwa nje wa mashindano ya kombe la Wanawake la Shirikisho la Soka nchini (FKF) dhidi ya Nakuru Metropolis Queens na Kipeed Queens (Ligi ya Taifa) mtawalia.

Vihiga kwa upande mwingine, walihakikisha wamevuna alama tatu muhimu kutoka kwa watani wao wa jadi Bunyore Starlets kwa kuwanyorosha 1-0. Bao hilo lilitiwa kimiani na kiungo Janet Moraa Bundi dakika ya saba.

Kwenye mechi nyingine ugani Camp Toyoyo jijini Nairobi, bao la Salano Jaef dakika ya 47 lilitosha kuwapa Nakuru Metropolis Queens alama tatu dhidi ya Kayole Starlets.

Nakuru wamesalia nafasi ya tano na alama 31 nao Kayole wamesalia mkiani na alama -9.

Ugani Mumias Complicated mjini Mumias kaunti ya Kakamega, Wadadia Girls waliwahangaisha Kisumu All starlets kwa kuwanyorosha 4-1.

Atsabina Laura alifunga mabao mawili dakika ya 30′ na 40′. Nae Jackline Chesang’ dakika ya 67’na 88′. Bao la Kisumu lilitiwa kimiani na Berverline Adika.

Wadadia walipiga hatua moja kwenye jedwali na kufunga tano bora na alama 29. Kisumu nao wameshikilia nafasi ya nane na alama 17.

[ad_2]

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Articles